Saturday, July 23, 2011

Zamaradi ‘awavua nguo’ mastaa Bongo

Imelda Mtema
Prisenta ‘sexy n’ hot’ wa Runinga na Radio Clouds FM, Zamaradi Mketema, ‘amewavua nguo’ laivu baadhi ya mastaa wa filamu za Kibongo ambao wamelewa umaarufu na kushindwa kutambua kuwa ni kioo cha jamii.

Zamaradi anayeendesha Programu ya Take-One kunako Clouds TV, alifunguka kuhusu ishu hiyo hivi karibuni kupitia ‘blog’ yake kuwa, kuna baadhi ya mastaa wa fani hiyo wamekuwa wakiweka bifu baada ya kuelezwa umuhimu wa wao kujiheshimu.

Alisema wasanii hao wamekuwa wakishindwa kuelewa kwamba wanapokosolewa ndiyo wanajifunza.

“Unajua bila vyombo vya habari kama magazeti, redio na televisheni, kazi zao ni bure, yaani ni kama kumkonyeza mtu gizani, sasa wanapoambiwa ukweli ni lazima waukubali na waufanyie kazi, siyo kuumia na kuwekeana bifu,” ilisomeka sehemu ya maelezo yake.

Zamaradi aliongeza kuwa, ni lazima wasanii waepukane na majivuno ambayo yanawafanya wasisonge mbele kisanii.

“Jamani mfano mzuri ni mwanadada Lady Jaydee (mwanamuziki Judith Wambura), hebu mwangalie alivyo, ana mafanikio makubwa lakini angekuwa na majigambo, leo hii asingekuwa na maendeleo kama aliyonayo,” alimalizia mjadala huo.

No comments:

Post a Comment