Friday, July 15, 2011

Miss Temeke kutifuana kesho!



Washiriki 16 wanaowania taji la kumtafuta mrembo wa Kitongoji cha Temeke jijini Dar es Salaam, wanatarajiwa kutifuana kesho ndani ya Ukumbi wa TCC Club uliopo Changombe katika kuwania Taji la Miss Temeke 2011.

Mratibu wa shindano hilo, Benny Kisaka alisema kuwa maandalizi yote juu ya shindano hilo yamekamilika kinachosubiriwa ni muda ufike.
“Kila kitu kiko sawa, warembo wako katika hali nzuri na kila mmoja ana uchu wa kuibuka mshindi, wapenzi wa urembo waje kwa wingi kushuhudia mtanange wa aina yake,” alisema Kisaka.

Aidha, alitamba kuwa kwa namna warembo wake walivyo wakali ana uhakika Miss Tanzania 2011 atatoka Temeke kama ilivyokuwa mwaka jana.

Shindano hilo litasindikwa na burudani ya kukata na shoka kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya Banana Zoro, AT na wengineo. 
 

No comments:

Post a Comment