
Ulimwengu wa mastaa wa Kibongo umejaa kila aina ya vitimbi, gumzo lililotawala kwa wale wa kike ni kunyoosheana vidole wao kwa wao kwa skendo ya uporaji wa waume za watu, Ijumaa lina ripoti kamili.
Wakipiga stori huku ‘shushushu’ wetu akiwasikiliza bila kujijua mara baada ya mazoezi ya netiboli ya timu yao ya Bongo Movies katika Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar es Salaam hivi karibuni, mastaa wawili (majina tunayo) walijikuta wakiingia kwenye mjadala mzito kuhusu skendo zinazoandikwa juu yao wakilaumiana kuwa hazileti picha nzuri kwa jamii.

“Unajua wanaume wanatuogopa sana wakihisi wakituoa nao watachafuka kwa kuambiwa wameoa makapi yaliyokubuhu kwa uporaji waume za watu.
“Shosti, mimi ninachoona hapa ni bora mtu ukajilinda usipatwe na aibu kama hiyo. Unajua inawezekana kabisa ndiyo sababu ya mastaa wengi kuchelewa kuolewa,” alisema mmoja wa wasanii hao chipukizi.

Akizungumza na Ijumaa juu ya ishu hiyo ya kupenda ‘kutoka’ na waume za watu, msanii Latifa Idabu ‘Badra’ wa Bongo Movies alikuwa na haya ya kusema:
“Kwa upande wangu, asikwambie mtu, naogopa sana kutembea na mwanaume wa mtu, nahisi siku waandishi wakiniandika kwa ishu hiyo nitazimia.”

AUNT EZEKIEL ‘GWANTWA’
Ni sura ya mauzo katika tasnia ya filamu za Kibongo, aliwahi kukumbwa na skendo ya ukwapuaji wa waume za watu wakiwemo, pedeshee Jack Pemba na Mwilu Mwilola ‘Silver’ huku akiapa kwamba hakuna kitu kitakachomuumiza kama ikitokea akaibiwa wa kwake kwani yeye amezoea kupora na siyo kuporwa.
NASREEN KARIM
Ni Miss Tanzania 2008/09, akiwa amevalia ‘krauni’ hiyo, skendo yake namba moja ilikuwa ni ya uporaji wa mume wa mtu ambaye ni mwimbaji wa Machozi Band, Mwinyigoha Ahmed.
ROSE NDAUKA
Anafanya vizuri katika Bongo Movies. Aliwahi kukumbwa na skendo ya kuvishwa pete na mume wa mtu huku akikanusha kuwa hakujua kuwa mwanaume huyo kutoka Tanga ni ‘mali’ ya mwanamke mwenzake.
ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’
Ni mhusika rasmi katika ‘kiwanda’ cha filamu za Kibongo. Hivi karibuni aliripotiwa kuchanwa viwembe kisa mume wa mtu. Alipofafanua skendo hiyo, alidai kwamba mwanaume aliyekuwa naye alikuwa rafiki wa kawaida hivyo mwenye mume alimhisi tu na si kweli kwamba alikuwa akitoka naye kimapenzi.

Haina ubishi kuwa anafunika ajabu katika Bongo Movies. Linapokuja suala la waume za watu, mwanamama huyo anakiri kwamba, yuko tayari ‘kutoka’ na kumzalia mtoto mwanaume yeyote kwa mkataba ilimradi tu awe na mkwanja bila kujali kama ni mume wa mtu au la.
BELINA MGENI
Ni modo the big name Bongo ambaye aliwahi kuripotiwa akidaiwa kuvishwa pete na mume wa mtu, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyetajwa kwa jina moja la Herman. Hata hivyo, Belina alitumia nguvu kubwa kukanusha ‘skandali’ hiyo.
ISSABELAH MPANDA
Alipata maujiko alipotwaa taji la Miss Ruvuma miaka ya nyuma. Miezi kadhaa iliyopita alijifungua mtoto wa kiume aliyempa jina la Obama ambaye kamwe hawezi kumwanika baba wa mtoto wake
No comments:
Post a Comment