Saturday, July 23, 2011

ABOUT ME.

Huwa naongea kuhusu wao then wanaongea kuhusu mimi wanakaza nikikaza wanajifanya mafisi I know whats this watoto wadogo ndio wanabebwa kwenye mapaja uko apo kiongozi?pamoja.

VIGOGO WAFURIKA

  • View GLOBAL's News

  • Na Imelda Mtema
    SHEREHE ya kuagwa ‘Sendoff’ ya dada wa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Vijana Mkoa wa Arusha, Catherine Magige, Jack Mjelwa ilikutanisha vigogo kibao wakiwemo viongozi mashuhuri nchini.
    Bakari Mwapachu (wa pili kulia) akijadiliana jambo katika sherehe hiyo.
    Katika sherehe hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, wiki iliyopita, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Raia, Bakari Mwapachu nao walitinga kwenye mnuso.

    Mh. Sitta (wa pili kulia) akiwa na mkewe, Margaret Sitta (kushoto).
    Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Magreth Sitta ambaye ni mke wa Sitta naye alikuwemo.

    Pamoja na kupambwa na vigogo, Catherine alifanya kufuru ya aina yake pale alipommwagia fedha

    Shilole ‘amtapika’ Barnaba


    Na Gladness Mallya
    MSANII wa filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ (pichani) amemtapika aliyekuwa mpenzi wake Elias Barnaba kwa madai kuwa hivi karibuni amemdhalilisha.  

    Akizungumza na Ijumaa juzi Shilole alisema kuwa, uhusiano wa kimapenzi kati yake na Barnaba haukuwa na kificho ila kwa kuwa ameonesha kutokuwa na msimamo, bora waachane tu.

    “Hakuna asiyejua kuwa Barnaba ni mpenzi wangu na yeye mwenyewe alikuwa anajitangaza na gari yangu alikuwa anaitumia na siku alipoondoka nilimsindikiza lakini nashangaa huku nyuma ameacha maneno mengi kuwa hawezi kutembea na mimi kwa sababu eti mimi ni mkubwa, nimeolewa na nina mtoto,” alisema Shilole.

    Aliendelea kudai kuwa, Barnaba ni mwanaume aliyezidiwa na tamaa na yeye ndiye aliyemchoka kwa hiyo anamsubiri akirudi kutoka Marekani, wanaachana rasmi.

    Katika siku za hivi karibuni Shilole na Barnaba wamekuwa wakidaiwa kuwa ni wapenzi lakini juzikati Barnaba aliruka kimanga na kudai kwamba hawezi kutoka na msanii huyo wa filamu kwani ni

    Zamaradi ‘awavua nguo’ mastaa Bongo

    Imelda Mtema
    Prisenta ‘sexy n’ hot’ wa Runinga na Radio Clouds FM, Zamaradi Mketema, ‘amewavua nguo’ laivu baadhi ya mastaa wa filamu za Kibongo ambao wamelewa umaarufu na kushindwa kutambua kuwa ni kioo cha jamii.

    Zamaradi anayeendesha Programu ya Take-One kunako Clouds TV, alifunguka kuhusu ishu hiyo hivi karibuni kupitia ‘blog’ yake kuwa, kuna baadhi ya mastaa wa fani hiyo wamekuwa wakiweka bifu baada ya kuelezwa umuhimu wa wao kujiheshimu.

    Alisema wasanii hao wamekuwa wakishindwa kuelewa kwamba wanapokosolewa ndiyo wanajifunza.

    “Unajua bila vyombo vya habari kama magazeti, redio na televisheni, kazi zao ni bure, yaani ni kama kumkonyeza mtu gizani, sasa wanapoambiwa ukweli ni lazima waukubali na waufanyie kazi, siyo kuumia na kuwekeana bifu,” ilisomeka sehemu ya maelezo yake.

    Zamaradi aliongeza kuwa, ni lazima wasanii waepukane na majivuno ambayo yanawafanya wasisonge mbele kisanii.

    “Jamani mfano mzuri ni mwanadada Lady Jaydee (mwanamuziki Judith Wambura), hebu mwangalie alivyo, ana mafanikio makubwa lakini angekuwa na majigambo, leo hii asingekuwa na maendeleo kama aliyonayo,” alimalizia mjadala huo.

    Saturday, July 16, 2011

    MZEE AVUNJA UKIMYA.

    huyu mzee alikuwa na n
    ngoja nikuonyeshe wewe kijana inaonyeha hunitambui
    ia gani?

    Linah ajimwaga The Atriums Hotel

    Esterlina Sanga ‘Linah’ akikamata 'menyu' na shabiki wake Damson Mnyenye ndani ya  Atriums Hotel.
    WIKI iliyopita staa wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linah’ alijimwaga  na shabiki wake namba moja, Damson Mnyenye, mkazi wa Ubungo,  Dar.

    Wawili hao ‘wali-injoi’ kinomanoma maakuli ya The Atriums Hotel hasa huduma za kistaa walizopatiwa na wahudumu nadhifu wa hoteli hiyo.

    Baada ya mpango mzima uliosababishwa na gazeti hili, Linah alifunguka: “Nimefurahia sana huduma za The Atriums Hotel, ni sehemu tulivu iliyojaa kila aina ya liwazo.”

    BOB JUNIOR AFUNIKA KWA MADEMU


    Na Musa Mateja, aliyekuwa Mbeya
    Msanii wa Bongo Fleva aliye pia ‘the big boss’ wa Sharobaro Records, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’ (pichani) amefunika ndani ya Jiji la Mbeya kwa kutembelewa na mademu hotelini alikofikia kwa ajili ya Tamasha la Fiesta.

    Ishu hiyo iliyoshuhudiwa na ‘vuvuzela’ wetu ilichukua nafasi ndani ya Hoteli ya Mount Stone, Mbeya mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo msanii huyo alikuwa mmoja wa wasanii ‘waliopafomu’ katika tamasha hilo.

    Baada ya kushtukia ishu hiyo, Amani lilitia maguu jirani na chumba cha Bob Junior kwa washkaji wengine ili kupata mkanda kamili ambapo lilikutana na majibu haya:

    “Wewe achana na Bob Junior, tangu tumefika ndiye anayeongoza kutembelewa na mademu chumbani.”

    Alipofuatwa ili kutoa ufafanuzi juu ya ishu hiyo, Bob Junior alifunguka:
    “Ni kweli wamenifuata mademu kibao lakini wengi ni wasanii wachanga wanahitaji

    WEMA AANIKA KALIO NJE!




    Miss Tanzania 2006/07 ambaye sasa amejikita kwenye uigizaji wa filamu, Wema Sepetu hivi karibuni alijikuta akilianika kalio lake alipokuwa mjini Morogoro.

    Tukio hilo la aibu lilijiri wakati mrembo huyo alipopanda jukwaani kumpa kampani laazizi wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’ alipokuwa akipafomu kwenye Tamasha la Fiesta lililofanyika ndani ya Uwanja wa Jamhuri.

    Wema ambaye alikuwa amevalia kigauni kifupi, awali alionekana akipanda jukwaani kuimba na Diamond wimbo wa Nitarejea lakini wakati akicheza, kigauni chake kilipanda juu hivyo kuianika sehemu hiyo nyeti.


    Kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya mashabiki kumzomea huku mwenyewe akidhani walikuwa wakimshangilia.

    Aidha, baadhi ya watu waliozungumza na Ijumaa uwanjani hapo walimlaumu Diamond kumpandisha mpenzi wake huyo jukwaani akiwa nusu uchi.
    “Hivi kweli wataoana hawa? Kama kweli wana nia ya dhati ya kuja kufunga ndoa, Diamond asingekubali mchumba wake apande jukwaani acheze makalio nje, hii ni aibu,” alisema Juma Kassim huku mwenzake.

    Hata hivyo, katika kuonesha kutojali, wawili hao walinaswa nyuma ya steji .wakipongezana kama walichokifanya ni chamsingi.

    Neno La Leo: Tanzania Ina vyote, Kasoro Watanzania!

    Ndugu zangu,
    Jana nilipokea barua kutoka kwa Mtanzania anayeishi Ujerumani. Barua hii imenigusa sana. Imechapwa kwa ujumla kwenye . Nitaweka hapa mwanzo tu wa barua husika, kisha nitayasema yangu.

    Namnukuu;

    “Salaam!
    Kaka yangu ,Tangu kuelewa kwangu ubovu huu wa serikali ya Tanzania nimekuwa nikilia kila siku ingawa mtu mzima machozi ni ngumu kutoka. Najipa moyo haya matatizo yataisha siku moja lakini naona sasa nakata tamaa. Hakuna uafadhali na kila siku zikienda ndio kwanza ufisadi unaimarika na mafisadi wanazaliwa pia.

    Najiuliza kuna mwisho wa haya? au natakiwa nifanyaje niache kulia? Niko Germany lakini huwa naona aibu nikiulizwa unatoka wapi? “ Mwisho wa nukuu.

    Naamini, kuwa nchi yetu ni tajiri sana, lakini watu wake ndio masikini sana. Ni wachache tu ndio wenye kunufaika na utajiri wa nchi yetu. Na jambo hilo hatupaswi tukaliacha liendelee. Angalia picha hizo; wakati Waziri wetu wa Nishati na Madini anaweza kuwa na muda wa kucheza densi kuna watoto wetu kule Songo Songo ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha huku eneo wanaloishi kuna wawekezaji wenye kuvuna gesi yetu na kujitengenezea faida kubwa, tena kwa kukwepa kulipa kodi.


    Na mkataba wao wa kuvuna gesi? Ni miaka 25! Robo karne nzima. Hao Watanzania wenzetu walioshiriki kuingia mikataba hii ya kifisadi huenda hawatakuwepo duniani baada ya robo karne ya wawekezaji kuchota na kukwangua gesi yetu asilia.


    Ndugu zangu,
    Rasilimali zetu tumeacha zisimamiwe na baadhi ya Watanzania wenzetu wenye hulka za mbweha. Ni watu wabinafsi na wasio na huruma kwa Watanzania wenzao.

    Ndio maana tunasikia kila kukicha kashfa zinazofuatana; Rada, Richmond, IPTL, EPA, Meremeta na nyinginezo nyingi. Ni kashfa zinazowafanya wachache wameremete huku wengi wakifubaa kwenye lindi la umasikini.


    Ndio, msingi wake ni ubaguzi wa kisiasa unaotokana na ubinafsi na tamaa ya mali kwa baadhi ya tuliowapa dhamana za kufanya maamuzi makubwa kwa niaba yetu. Ni hali ya baadhi ya tuliowapa dhamana za uongozi kuishiwa chembe chembe za uzalendo; mapenzi kwa nchi yao.Ni watu wenye kulinda maslahi yao na ya wanaowazunguka. Wako tayari hata kutumia mbinu za Umafia kutimiza malengo yao.



    Watanzania wengi sasa wanaopoteza moyo wa uzalendo kwa nchi yao. Kuna hata wenye kufikia kutamka; "Nchi hii ina wenyewe". Kuna anayetamka hilo kwa lengo la kumtishia mwenzake au kulazimisha kitu fulani kifanyike. Lakini, kuna wenye kutamka hivyo kuashiria kukata tamaa. Kuwa hata wafanye nini, hakuna anayewasikiliza ama kuwajali. Hizi si dalili njema kwa taifa.

    Kuna wanaoiba mali ya umma mchana wa jua kali. Hakuna anayewagusa. Ukiuliza utajibiwa; “Ah! Nchi ina wenyewe!”. Kwamba kuna baadhi yetu hawajisikii kuguswa na nchi hii, hawajisikii kuwa na nguvu ya kupiga vita maovu yanayotusumbua. Baadhi yetu wameanza kupungukiwa na mapenzi na nchi yao. Ni hatari.

    Tuna lazima ya kuwa na ujasiri wa kupigania maslahi ya nchi yetu. Ni heri kufa kwa kupigwa risasi kuliko fedheha ya kufa kwa kuumwa na mbu wa Malaria katika nchi ambayo ina rasilimali za kutuwezesha kujenga uwezo wa kuangamiza malaria. Lakini, tunakubali wachache miongoni mwetu wahujumu rasilimali zetu.

    Juni 16, 2004 nilipata kuandika hili kwenye gazeti la Majira; kuwa Tanzania ina vyote, kasoro Watanzania. Niliandika; kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana. Ni nchi ya kujivunia. Kwamba Tanzania ni nchi kubwa sana kwa eneo. Ni nchi yenye rasilimali nyingi; ardhi yenye rutuba, mito, maziwa, milima, mabonde, bahari na vivutio vingi vya asili. Hata hivyo, Tanzania ni moja ya nchi masikini sana duniani. Kwa nini?

    Ndio, kikubwa kinachokosekana Tanzania ni Watanzania. Tanzania tunayoijenga sasa ni mkusanyiko tu wa watu wa makundi mbali mbali wenye kwenda kwa staili ya 'kila mtu na lwake'. idadi ya Watanzania wenye uzalendo na mapenzi kwa nchi yao inazidi kupungua. Ubinafsi umekithiri, na ubinafsi mbaya zaidi ni ule wenye kufanywa na

    VODACOM YAANDAA AEROBIC DAY KWA WAREMBO


    Warembo wanaoshiriki Vodacom Miss Ilala na Kinondoni wakiwa katika mazoezi ya viungo ya pamoja yaliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa mashindano hayo Vodacom Tanzania katika viwanja vya Kijitonyama jijini Dar es Salaam. PICHANI Mmoja wa walimu wa maoezi ya viungo kutoka Gym ya Genesis iliyopo Kijitonyama akitoa mazoezi ya viungo kwa warembo hao.

    Friday, July 15, 2011

    Mastaa hatari kwa waume za watu

    Na Mwandishi Wetu
    Ulimwengu wa mastaa wa Kibongo umejaa kila aina ya vitimbi, gumzo lililotawala kwa wale wa kike ni kunyoosheana vidole wao kwa wao kwa skendo ya uporaji wa waume za watu, Ijumaa lina ripoti kamili.

    Wakipiga stori huku ‘shushushu’ wetu akiwasikiliza bila kujijua mara baada ya mazoezi ya netiboli ya timu yao ya Bongo Movies katika Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar es Salaam hivi karibuni, mastaa wawili (majina tunayo) walijikuta wakiingia kwenye mjadala mzito kuhusu skendo zinazoandikwa juu yao wakilaumiana kuwa hazileti picha nzuri kwa jamii.
    Huku wakiperuzi na kudadisi moja ya magazeti pendwa lililobeba habari iliyokuwa ikiponda tabia zao za kupenda kudandia waume za watu, mastaa hao waliapa kujilinda na skendo ya aina hiyo kwani inatia doa hata kwa wanaume wanaojitokeza kutaka kuwaoa.

    “Unajua wanaume wanatuogopa sana wakihisi wakituoa nao watachafuka kwa kuambiwa wameoa makapi yaliyokubuhu kwa uporaji waume za watu.

    “Shosti, mimi ninachoona hapa ni bora mtu ukajilinda usipatwe na aibu kama hiyo. Unajua inawezekana kabisa ndiyo sababu ya mastaa wengi kuchelewa kuolewa,” alisema mmoja wa wasanii hao chipukizi.
    Hivi karibuni, staa wa tasnia hiyo, Blandina Chagula ‘Johari’ alikaririwa akisema kuwa, wanaume wanaogopa kumuoa akihisi kuwa hali hiyo inatokana na skendo za baadhi ya wasanii hao.

    Akizungumza na Ijumaa juu ya ishu hiyo ya kupenda ‘kutoka’ na waume za watu, msanii Latifa Idabu ‘Badra’ wa Bongo Movies alikuwa na haya ya kusema:

    “Kwa upande wangu, asikwambie mtu, naogopa sana kutembea na mwanaume wa mtu, nahisi siku waandishi wakiniandika kwa ishu hiyo nitazimia.”
    Katika uchunguzi makini wa The Udaku Master, Ijumaa, listi ya mastaa hatari waliowahi kukumbwa na skendo ya aina hiyo ni ndefu, hapa linakumegea baadhi yao;

    AUNT EZEKIEL ‘GWANTWA’
    Ni sura ya mauzo katika tasnia ya filamu za Kibongo, aliwahi kukumbwa na skendo ya ukwapuaji wa waume za watu wakiwemo, pedeshee Jack Pemba na Mwilu Mwilola ‘Silver’ huku akiapa kwamba hakuna kitu kitakachomuumiza kama ikitokea akaibiwa wa kwake kwani yeye amezoea kupora na siyo kuporwa.

    NASREEN KARIM
    Ni Miss Tanzania 2008/09, akiwa amevalia ‘krauni’ hiyo, skendo yake namba moja ilikuwa ni ya uporaji wa mume wa mtu ambaye ni mwimbaji wa Machozi Band, Mwinyigoha Ahmed.

    ROSE NDAUKA
    Anafanya vizuri katika Bongo Movies. Aliwahi kukumbwa na skendo ya kuvishwa pete na mume wa mtu huku akikanusha kuwa hakujua kuwa mwanaume huyo kutoka Tanga ni ‘mali’ ya mwanamke mwenzake.

    ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’
    Ni mhusika rasmi katika ‘kiwanda’ cha filamu za Kibongo. Hivi karibuni aliripotiwa kuchanwa viwembe kisa mume wa mtu. Alipofafanua skendo hiyo, alidai kwamba mwanaume aliyekuwa naye alikuwa rafiki wa kawaida hivyo mwenye mume alimhisi tu na si kweli kwamba alikuwa akitoka naye kimapenzi.
    JACQUELINE PENTZEL ‘JACK WA CHUZ’
    Haina ubishi kuwa anafunika ajabu katika Bongo Movies. Linapokuja suala la waume za watu, mwanamama huyo anakiri kwamba, yuko tayari ‘kutoka’ na kumzalia mtoto mwanaume yeyote kwa mkataba ilimradi tu awe na mkwanja bila kujali kama ni mume wa mtu au la.

    BELINA MGENI
    Ni modo the big name Bongo ambaye aliwahi kuripotiwa akidaiwa kuvishwa pete na mume wa mtu, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyetajwa kwa jina moja la Herman. Hata hivyo, Belina alitumia nguvu kubwa kukanusha ‘skandali’ hiyo.

    ISSABELAH MPANDA
    Alipata maujiko alipotwaa taji la Miss Ruvuma miaka ya nyuma. Miezi kadhaa iliyopita alijifungua mtoto wa kiume aliyempa jina la Obama ambaye kamwe hawezi kumwanika baba wa mtoto wake

    Miss Temeke kutifuana kesho!



    Washiriki 16 wanaowania taji la kumtafuta mrembo wa Kitongoji cha Temeke jijini Dar es Salaam, wanatarajiwa kutifuana kesho ndani ya Ukumbi wa TCC Club uliopo Changombe katika kuwania Taji la Miss Temeke 2011.

    Mratibu wa shindano hilo, Benny Kisaka alisema kuwa maandalizi yote juu ya shindano hilo yamekamilika kinachosubiriwa ni muda ufike.
    “Kila kitu kiko sawa, warembo wako katika hali nzuri na kila mmoja ana uchu wa kuibuka mshindi, wapenzi wa urembo waje kwa wingi kushuhudia mtanange wa aina yake,” alisema Kisaka.

    Aidha, alitamba kuwa kwa namna warembo wake walivyo wakali ana uhakika Miss Tanzania 2011 atatoka Temeke kama ilivyokuwa mwaka jana.

    Shindano hilo litasindikwa na burudani ya kukata na shoka kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya Banana Zoro, AT na wengineo. 
     

    Thursday, July 14, 2011

    conglatulation

    nawatakia mtihani mwema wanafunzi wotewa AMUCTA.mungu atubariki.

    Wednesday, July 13, 2011

    Monalisa amkimbia Rais Kikwete!



    STAA katika tasnia ya filamu Bongo, Yvonne Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’, Julai 6, mwaka huu ndani ya Viwanja vya Sabasaba, Mtoni jijini Dar es Salaam alitimua mbio kumkimbia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

    Monalisa alikuwa kama mtu aliyepandwa na malaria ya ghafla kichwani pale alipomuona ‘laivu’ Rais Kikwete alipokuwa akitembelea mabanda katika viwanja hivyo.

    Monalisa akiwa na mama yake, Suzan Lewis ‘Natasha’ pamoja na wasanii wengine waliokuwa kwenye banda la Dk. Rahabu, alitimua mbio baada ya kumuona Rais Kikwete akiwa anatokea mbele yao, akiwa na wapambe wake.
    “Kwanza sikutarajia kumuoa rais, hivyo nilipomuona nilipatwa na mshtuko, ikanibidi nikimbie,” alijitetea.

    Monalisa pia alisema kuwa rais anatisha kutokana na dola inayomzunguka kiasi cha kufanya watu kutishika na kudhani kuwa siyo mtu wa kawaida.

    Baadhi ya watu waliokuwepo eneo hilo waliangua vicheko lakini wengine walimuonea huruma kwa jinsi alivyokosa amani na kukimbia.

    Penzi la H. Baba



    PENZI la mastaa wawili wanaotamba katika tasnia za filamu na muziki Bongo, Hamis Ramadhani Baba ‘H Baba’ na Frola Mvungi limeanza kuchokonolewa na kudaiwa kufanyiwa mambo  ya kishirikina, Risasi Mchanganyiko lina taarifa.

    Akizungumza na gazeti hili Jumapili iliyopita katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam, H Baba alisema kuwa, amekumbana na mambo mengi katika uhusiano wake na diva huyo wa filamu.

    H Baba.
    “Kuna mambo mengi sana nyuma ya pazia ambayo watu hawayajui na kama nisingekuwa mvumilivu ningekuwa nimeshaachana na Flora, “ alisema H Baba.

    Mwanamuziki huyo wa Bongo Fleva ambaye pia huigiza filamu, alitoboa kuwa kuna watu wamefikia kuwaendea kwa waganga ili kulivunja penzi lao lakini wanagonga mwamba.

    “Yaani kila siku watu wanatutafuta, wengine nawajua kabisa kwa majina, wanajaribu hata kwenda kwa babu ili watuharibie kitu ambacho naamini watajihangaisha bure, mimi namwamini Mungu,” alisema H Baba.
    Boniface Ambani.
    Mbali ni hilo, H Baba alisema kuwa, mara kadhaa amekuwa akikuta meseji  katika simu ya mpenzi wake huyo kutoka kwa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Boniface Ambani.

    “Ambani bado anamsumbua Frola kwani amekuwa akimpigia simu na hata kumtumia SMS  za kumshawishi kimapenzi lakini mimi ninanyamaza kimya tu,” alisema.

    Waandishi wetu walipomuuliza H Baba kwamba ni lini wanatarajia kufunga ndoa na Flora, alisema kuwa kwa sasa bado hawajafikia hatua hiyo.

    “Bado naendelea kumchunguza, siwezi kumuoa leo wala kesho, unajua  mnaweza kukurupuka kuoana kisha

    MWAUNAUME MWENYE SIFA HIZI MPE POLE

    KALENDA yangu inanionesha kuwa leo ni Jumatano, Julai 13, 2011. Hakika siku zinakwenda kasi sana, tayari tumeshaanza nusu nyingine ya mwaka. Karibuni marafiki uwanjani tujifunze mambo mbalimbali kuhusu uhusiano na mapenzi kama ilivyo ada.
    Kabla ya kuingia rasmi katika mwendelezo wa mada yetu ambayo ilianza wiki iliyopita juu ya mwanaume sahihi wa kumpa moyo wako, napenda kutoa changamoto kwenu marafiki zangu.

    Siku inapoondoka inakuwa imekwenda, haiwezi kurudi tena. Umakini katika kila kitu unachokifanya katika maisha ni jambo muhimu sana marafiki. Hebu jiulizeni, tukiwa tumeshaanza nusu nyingine ya mwaka, mmefanya nini?

    mna mafanikio gani katika kipindi cha nusu mwaka kilichopita?
    Je, mnaishi mkiwa na mipango ambayo mnaitekeleza au mnakwenda tu, mradi siku zinakwenda? Ishini kwa mipango rafiki zangu, siku ikiondoka, hakuna nyingine tena kama hiyo.

    Hata katika mapenzi, unapaswa kujiuliza, umefanya nini kwa mpenzi wako? Je, umekuwa hodari wa kupanga wenzi wengi au umedumu na yule uliyekuwa naye tangu mwaka jana? Makosa madogo yanayotokea katika uhusiano wenu, umeyaweka sawa au ndiyo umeona uamuzi wa kuachana ni bora zaidi?

    Kuwa na wapenzi wengi si ujanja, kubadilisha wenzi kila siku si kigezo cha kukufanya uonekane mwerevu! Rafiki yangu, lazima uwe makini kuhakikisha uhusiano wako unaendelea kuwa wenye nguvu kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele.

    Wale mliopo kwenye ndoa, mnatakiwa kufahamu kwamba ugomvi si kitu cha kuendekeza. Kupishana kiswahili ndani ya nyumba ni jambo la kawaida, muhimu hapa ni kuangalia namna mnavyokabiliana na changamoto hizo na maisha kuendelea kama kawaida.

    Acha usiri kwa mwenzi wako, kama mnaishi ndani ya ndoa ni lazima muwe wamoja mkielezana ukweli wa kila kinachotokea katika maisha ya kawaida. Kama kuna jambo la maendeleo unataka kulifanya, usifanye kimya kimya, kaa chini na mwenzako mjadiliane.

    Kwa kufanya hivyo, uhusiano wenu utazidi kuwa wenye nguvu zaidi na mafanikio makubwa yatakuwa ndiyo zawadi ya mapenzi yenu. Rafiki zangu, hizo ni dondoo tu za kumaliza nusu ya mwaka, sasa tuendelee na mada yetu.

    Si kila mwanaume anaweza kuwa mume, wengine wana tabia chafu ambazo kama hutakuwa makini utagundua ukiwa tayari umeshaingia kwenye kifungo cha ndoa, ambapo hapo sasa hutaweza kutoka tena.

    Kama mtakumbuka vizuri, wiki iliyopita nilianza kwa kuelezea baadhi ya vigezo muhimu vya kuzingatia kwa mwanaume ambaye anafaa kuwa wa maisha. Nilisema aliye mkweli, anayekujali na mwenye msimamo.

    Kila kipengele nilikifafanua kwa marefu na mapana, leo tunamalizia vipengele vilivyosalia, nikiamini kwamba vitakupa tiba katika kufanya maamuzi sahihi kwenye uhusiano wako.

    ANAYESHAURIKA
    Mwanaume ambaye anafaa kuwa baba bora wa familia ni yule ambaye anakubali mawazo ya mwenzake. Anakubali ushauri. Siku zote amekuwa mkweli kwako, anakubayanisha mali zake pamoja na biashara anazofanya.

    Haoni vibaya kukufundisha juu ya kuendesha mali zake. Inapotokea unamshauri, hukusikiliza kwa umakini na kuyafanyia kazi mawazo yako. Hata kama akiona ushauri wako si wa busara sana au akawa na mashaka nao, hutulia na kupima maneno yako kwa umakini kabla hajayafanyia kazi.

    Ni vema mwanaume ashaurike (inapobidi) ili  asifanye madhara katika maamuzi ya familia kwa kusingizio cha ubaba ndiyo kichwa ca familia. Dalili za udikteta kama anazo utaziona mapema sana katika kipindi cha urafiki wenu.

    Kama ana tabia hiyo ni wazi kwamba hata mkiwa kwenye ndoa, utakuwa msindikizaji tu; mawazo yako hayatathaminiwa na mchango wako hautaonekana.

    ANAJALI NDUGU ZAKO
    Hapa nazungumza zaidi na wale ambao uhusiano wao tayari unajulikana. Wazazi wa pande zote wanaufahamu. Kama ndivyo ni lazima mwanaume wako awe na upendo na ndugu, jamaa na marafiki zako.

    Kuna msemo wa Kiswahili unasema `ukipenda boga, penda na lake’ na msemo mwingine unaofanana na huo unasema `unapopenda jipu penda na usaha wake’ kwa wakati mmoja, misemo hii inasisitiza upendo.

    Kwamba kuna vipimo kadhaa vya upendo lakini moja ni kumwangalia kama ana upendo kwa ndugu zako. Mwanaume huyu mara zote huulizia hali za wazee wako pamoja na ndugu zako wengine.

    Hii ni sawa na mawingu kabla ya mvua. Kwa sababu kama atashindwa kuwajali ndugu zako japo kwa kuwajulia hali wakati huu, utakapoingia katika ndoa atakuruhusu ukawasabahi kweli?
    Rafiki zangu, zipo sifa nyingi sana za kuangalia lakini hizi ni zile muhimu zaidi, ambazo kama mwanaume wako anazo, basi ni ruksa kumpa moyo wako wote. Mada imeisha.

    Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi ambaye anaandikia magazeti ya , ameandika vitabu vya True Love na Let’s Talk About Love. Unaweza kumtembelea kwenye mtandao wake;  HYPERLINK “

    ISHA MASHAUZI, KHADIJA KOPA WAPAGAWISHA WABUNGE DOM

    Isha Mashauzi (kulia) akicheza kiduku na mama yake.
    ...Wabunge wakiserebuka.
    WAIMBAJI mahiri wa muziki wa taarabu nchini, Isha Ramadhani (Mashauzi) na ‘Malkia wa Mipasho’, Khadija Omary Kopa, wiki iliyopita waliwapagawisha wabunge mjini Dodoma katika sherehe ya ‘Kitchen Party’  ya dada wa Mh. Catherine Magige (Mbunge wa CCM), aitwaye Jacqueline Mjelwa, iliyofanyika katika ukumbi wa African Dreams.

    Mh. Magige (katikati) akiingia ukumbini na mama yake mzazi.
    Waziri wa Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia (kushoto), akiongoza mduara kwa wabunge.
    Isha Mashauzi (kulia), mama yake (katikati) na MC Kide wakifanya mambo yao.
    Magige akiongea jambo. Katikati ni dada yake.
    Aliyewahi kuwa waziri wa elimu, Margaret Sitta, akiwasalimia waliohudhuria.
    Khadija Kopa katika pozi.
    Magige na Mh. Subira  wakisakata rumba.
    Mh. Anna Muonga katika pozi.
    Mh. Grace Kiwelu pia alikuwepo.
    Wabunge wakijinafasi.
    Mkazi wa Dar, Mboni Masimbe, akifurahia maisha.
    Magige katika pozi.
    Wabunge katika picha ya pamoja.

    DK BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TATU WA BARAZA LA WAKUU WA VYUO VIKUU HURIA AFRIKA

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mhadhiri Chuo Kikuu Huria cha Zanzibar Tanzania, Grace Kissassi, wakati alipokutana naye baada ya kufungua rasmi mkutano mkuu wa 3 wa Baraza la wakuu wa Vyuo Vikuu huria kutoka Afrika, kuhusu elimu ya mafunzo ya masafa uliofunguliwa rasmi leo  Julai 13, 2011 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa. Pichani juu: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa 3 wa Baraza la Wakuu wa Vyuo Vikuu huria kutoka Afrika baada ya kuzindua mkutano huo kuhusu mafunzo ya Elimu ya Masafa, leo Julai 13 jijini Dar es Salaam.

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa siku 3, kuhusu mafunzo ya Elimu ya Masafa unaowashirikisha wakuu wa Vyuo Vikuu Huria kutoka nchi za Afrika, uliofunguliwa leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.